Home Sports SAIDO AWASHUKURU NBC KWA TUZO

SAIDO AWASHUKURU NBC KWA TUZO

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ ameishukuru Benki ya NBC kwa kutoa motisha kwa wachezaji, huku akiamini hiyo inasaidia kujituma zaidi uwanjani.

 

Saido aliyasema hayo baada ya hivi karibuni kupokea tuzo yake ya Mchezaji Bora wa mwezi Februari wa Ligi Kuu Bara msimu huu sambamba na shilingi milioni moja kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo, Benki ya Taifa ya Biashara (NBC).

 

Katika tukio hilo lililofanyika Uwanja wa Azam Complex, Dar, Jumatano ya wiki hii, wadhamini hao wakuu wa Ligi Kuu Tanzania Bara pia walimkabidhi mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele Tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi Januari, sambamba na ile ya Kocha Bora wa mwezi Februari iliyokwenda kwa Nasreddine  Nabi wa Yanga.

 

Mayele, Saido na Nabi, walikabidhiwa zawadi zao za tuzo na mfano wa hundi ya shilingi milioni moja kwa kila mmoja na Mfanyakazi wa Kitengo cha Masoko NBC, David Raymond.

Previous articleARTETA:TULIKUWA NA KILA KITU CHAKUSHINDA,SPIDI TATIZO
Next articleSIMBA QUEENS WANATAKA ALAMA TATU