KAGERA SUGAR YAANZA KWA MWENDO WA KUSUASUA
FUNDO za walima miwa Kagera Sugar zinakatwa na wapinzani wao kila wanaposhuka uwanjani kwa kukwama kukomba pointi kwenye mechi mbili mfululizo za ligi ambazo ni dakika 180. Kagera Sugar chini ya Kocha Mkuu, Mecky Maxime kete yake ya kwanza ilikuwa Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma dhidi ya Mashujaa ilishuhudia ubao ukisoma Mashujaa 2-0 Kagera Sugar….