Home Sports SIMBA YAKOMBA POINTI TATU MBELE YA WALIMA ZABABI

SIMBA YAKOMBA POINTI TATU MBELE YA WALIMA ZABABI

UBAO wa Uwanja wa Uhuru Agosti 20 baada ya dakika 90 za jasho wa wanaume 22 kusaka pointi tatu umesoma Simba 2-0 Dodoma Jiji.

Mabao ya Simba ya pira Uturuki yamefungwa katika vipindi viwili tofauti, dakika ya 43 kupitia kwa Jean Baleke ambaye alikuwa wa kwanza kuwatungua wazee wa pira Zabibu.

Kipindi cha pili ni dakika ya 55 Simba ilipachika bao la pili kupitia kwa Moses Phiri ambaye aliingia kipindi cha pili akitokea benchi.

Dodoma Jiji mbinu ya kuwalinda mbele ya Simba imewapunguzua idadi ya mabao ya kufungwa huku wakikwama kuwatungua Simba kwa kukosa utulivu kupitia nafasi ambazo walizipata.

Hata Simba licha ya kuwa nyumbani bado safu yake ya ushambuliaji kwenye eneo la umaliziaji kwenye mchezo huo wa ligi.

Previous articleNANI KUVUNJA REKODI YA MAYELE YANGA?
Next articleDANADANA ZA LAVIA ZIMEGOTA MWISHO, LIVERPOOL NDO BASI