DANADANA ZA LAVIA ZIMEGOTA MWISHO, LIVERPOOL NDO BASI

  BAADA ya danadana za kutosha, hatimaye Chelsea imekamilisha usajili wa kiungo rasta, Romeo Lavia kutoka Southampton.

  Kiungo huyo kinda ambaye timu yake ya Southampton ilishuka daraja msimu uliopita alikuwa akitakiwa kwa ukaribu zaidi na Liverpool lakini akachagua Chelsea ambayo amejiunga nayo kwa ada ya pauni mil 53 kukiwa na nyongeza ya pauni mil 5.

  Lavia anaenda kuungana na Moises Caicedo, ambaye Liverpool pia walimtaka lakini wakamkosa katika dau la rekodi ya Uingereza ya pauni milioni 115 huku Mauricio
  Pochettino akiimarisha zaidi eneo lake la kiungo.

  Lavia alijiunga na Southampton kutoka Manchester City miezi 12 iliyopita na mabingwa hao wanatarajiwa kupata asilimia 20 ambayo ni pauni 10.6m ya awali kutokana na kifungu cha mauzo.

  Lavia amesaini mkataba wa miaka saba na atavaa jezi namba 45. Mkataba wake utamfanya apate kitita cha
  pauni 100,000 kwa wiki.

  Amesema, “Nina furaha sana kujiunga na Chelsea na kuwa sehemu ya mradi huu wa kusisimua. Ni klabu ya soka yenye historia nzuri na nina furaha sana kuanza.”

  Previous articleSIMBA YAKOMBA POINTI TATU MBELE YA WALIMA ZABABI
  Next articleYANGA YAFANYA KWELI KIMATAIFA