Home Sports YANGA YAFANYA KWELI KIMATAIFA

YANGA YAFANYA KWELI KIMATAIFA

UKIWA ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Uwanja wa Azam Complex Yanga wamepeta kwa kufanya kweli katika mchezo wa awali uliochezwa Agosti 20.

Kukiwa na mabadiliko kwenye kikosi cha Miguel Gamondi pamoja na aina ya uchezaji mchezo huo baada ya dakika 90 ubao umesoma ASAS Djibouti 0-2 Yanga.

Ni Aziz Ki dakika ya 22 alipachika bao la kuogoza akiwa ndani ya 18 kwa wapinzani wao na kuipa Yanga bao la kuongoza kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili ni Kennedy Musonda akapigila chuma cha pili dakika ya 53 kwenye mchezo huo.

Mchezo ujao kimataifa kwa Yanga unatarajiwa kuchezwa kwa mara nyingine Uwanja wa Azam Complex na Yanga watakuwa wenyeji wa mchezo huo.

Previous articleDANADANA ZA LAVIA ZIMEGOTA MWISHO, LIVERPOOL NDO BASI
Next articleAZAM FC WAANZA KWA KUPOTEZA UGENINI KIMATAIFA