Home Sports VIDEO: SIMBA YAFUNGUKIA ISHU YA PHIRI NA KUFUNGA

VIDEO: SIMBA YAFUNGUKIA ISHU YA PHIRI NA KUFUNGA

UONGOZI wa Simba umezungumzia juu ya nyota wao Moses Phiri kurejea katika kikosi na kufunga katika mchezo wa ligi.

Phiri anatambua kwamba msimu wa 2022/23 ni Saido Ntianzokiza wanayecheza naye kikosi kimoja pamoja na Fiston Mayele aliyekuwa ndani ya Yanga walitwaa tuzo ya ufungaji bora.

Nyota huyo wakati msimu unaanza alikuwa anakimbizana na Mayele wa Yanga kwenye suala la ufungaji alipopata maumivu hakuwa kwenye ubora wake na kumuacha mzee wa kutetema akiwatetemesha mashabiki wa Yanga.

Agosti 20 alifungua akaunti ya mabao Phiri kwa kufunga mbele ya Dodoma Jiji mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru jambo lililomuibua Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba.

Previous articleLIGI IMEANZA NA UKIMYA, WAAMUZI MSINYONGE HADHARANI TENA
Next articleROBERTINHO ATEMA CHECHE, GAMONDI ALIREJESHA KUNDINI JEMBE