Home Sports SIMBA 1-0 DODOMA JIJI, UWANJA WA UHURU WANAPATA TABU

SIMBA 1-0 DODOMA JIJI, UWANJA WA UHURU WANAPATA TABU

LINAPIGWA pira Uturuki v Pira Zabibu Uwanja wa Uhuru huku ukuta wa Dodoma Jiji ukiwa imara kuwakabili wapinzani wao.

Licha ya nguvu walizonazo Dodoma Jiji kuwazuia washambuliaji wa Simba wakiongozwa na Jean Baleke ni mashuhuda ubao ukisoma Simba 1-0 Dodoma Jiji.

Jean Baleke ametupia bao dakika ya 43 kwenye Uwanja wa Uhuru ambao timu zote zinaonekana kupata tabu kucheza katika uwanja huo.

Simba katika nafasi sita ambazo zimelenga lango moja pekee imezama nyavuni huku Dodoma Jiji wakiwa hawajapiga shuti lililolenga lango kwa Ally Salim katika dakika 45 za mwanzo.

Previous articleMASTAA SIMBA WATATU MAJANGA
Next articleNANI KUVUNJA REKODI YA MAYELE YANGA?