Home Sports AJIBU AFUNGA BAO LA AJABU KINOMANOMA

AJIBU AFUNGA BAO LA AJABU KINOMANOMA

MSIMU wa 2023/24 bao la ajabu na nzuri limefungwa ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2023/24.

Ipo wazi kwamba ni Yanga wanatetea taji la ubingwa baada ya kutwaa msimu wa 2022/23.

Coastal Union ya Tanga ni mashuhuda wa Yanga wakitwaa ubingwa na msimu huu wameanza kwa kupoteza mchezo wa kwanza na ule wa pili wakiambulia pointu moja ugenini.

Agosti 20, 2023 ukiwa ni mchezo wa pili Ibrahim Ajibu nahodha wa Coastal Union amefungua akaunti yake ya mabao akiwa na uzi mpya kwa kufunga bao la ajabu akiwa nje 18.

Ikumbukwe kwamba Ajibu kwa nyakati tofauti amecheza ndani ya Yanga, Simba, Azam FC na Singida Fountain Gate.

Ni jana katika mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar uliochezwa Uwanja wa Manungu ilikuwa dakika ya 70 Ajibu alipiga faulo hiyo kwa mguu wake wa kulia ikamshinda mlinda mlango wa Mtibwa Sugar.

Licha ya bao hilo la Ajiu dakika ya 70, Mtibwa Sugar walijibu mapigo dakika ya 84 walipachika bao la kuweka usawa na kufanya ubao kusoma Mtibwa Sugar 1-1 Coastal Union.

 

Previous articleHAWA YANGA WANA BALAA, PHIRI AVUNJA UKIMYA SIMBA
Next articleBEACH SOCCER NI MWENDO WA VICHAPO TU