Home International MASHUJAA NI MASHUJAA KATIKA KAZI NYINGINE

MASHUJAA NI MASHUJAA KATIKA KAZI NYINGINE

BAADA ya kufungua kete ya kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara kishujaa kwa kupata ushindi dhidi ya Kagera Sugar, Mashujaa FC ya Kigoma leo ina kibarua kingine cha kufanya.

Ipo wazi kuwa mabingwa wa ligi ni Yanga wana kibarua cha kutetea taji hilo kwa msimu wa 2023/24.

Bado Yanga haijashuka uwanjani kutokana na kuwa na majukumu ya kimataifa na mchezo wao wa kwanza unatarajiwa kuchezwa Agosti 23, Uwanja wa Azam Complex.

Yanga wao kete yao itakuwa dhidi ya KMC kwa msimu wa 2023/24.

Mashujaa imepanda ligi msimu huu ipo chini ya Kocha Mkuu, Mohamed Abdalah, (Bares) ilikomba pointi tatu Agosti 16, Agosti 21 ina kibarua kingine cha kusaka pointi tatu dhidi ya Geita Gold.

Ikumbukwe kwamba timu zote zimetoka kushinda mechi zao za ufunguzi, Geita Gold wao waliitungua Ihefu Uwanja wa Highland Estate bao moja na kukomba pointi tatu.

Bares amesema kuwa wana kazi kubwa ya kufanya kwenye mchezo huo kupata pointi tatu kutokana na ushindani uliopo.

“Tunawaheshimu wapinzani wetu na tunajua kwamba mchezo utakuwa mgumu tupo tayari kwa mchezo huo kupata pointi tatu,”.

Previous articleAZAM FC WAANZA KWA KUPOTEZA UGENINI KIMATAIFA
Next articleHAWA YANGA WANA BALAA, PHIRI AVUNJA UKIMYA SIMBA