
KIGOGO YANGA AFICHUA SIRI, WINGA MGHANA KATIKA RADA ZA SIMBA
KIGOGO Yanga afichua siri, Simba yampa Mkude heshima yake ndani ya Spoti Xtra, Alhamisi
KIGOGO Yanga afichua siri, Simba yampa Mkude heshima yake ndani ya Spoti Xtra, Alhamisi
MWAMBA Daniel Amoah beki wakuaminika ndani ya kikosi cha Azam FC bado yupo ndani ya Azam FC baada ya kuongeza dili la mwaka mmoja. Nyota huyo anaingia kwenye orodha ya waliomtungua Djigui Diarra, ‘Screen Protecta’ kipa namba moja wa Yanga kwenye Mzizima Dabi, Uwanja wa Mkapa ubao uliposoma Azam FC 2-2 Yanga. Amoah ni mechi…
RASMI kiungo Djibril Sillah nyota wa Gambia ni ingizo jipya ndani ya Azam FC. Kiungo huyo anakuja kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho ambacho kimekosa ubingwa msimu wa 2022/23 ambao umekwenda Yanga. Taarifa rasmi iliyotolewa na Azam FC imeweka wazi kuwa wamefikia makubaliano na Klabu ya RS Berkane kumnunua kiungo huyo mshambuliaji Raia huyo wa Gambia…
JEMBE afichua suala la kiungo wa zamani wa Simba, Jonas Mkude kusajiliwa Yanga baada ya kuachana na Simba. Mkude ni Legend ambaye amedumu kwa muda ndani ya kikosi cha Simba ambacho kwa sasa kinanolewa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira
PAPE Malickou Ndoye nyota wa Azam FC ameongeza mkataba wa mwaka mmoja kubaki ndani ya timu hiyo. Nyota huyo raia wa Senegal amekuwa na kazi kubwa katika timu hiyo ambayo imekamilisha ligi ikiwa nafasi ya tatu. Taarifa rasmi kutoka ndani ya Azam FC imeeleza kuwa nyota huyo ambaye ni beki kitasa bado yupo ndani ya…
SIMBA mpya usipime, huyu Gamondi ni Nabi mtupu ndani ya Championi Jumatano
MATESO makubwa ambayo yanatokea kwa viongozi kushindwa kutimiza ahadi zao yanawatesa mpaka mashabiki kutokana na matokeo kuwa mabaya. Kwa yale ambayo yamepita msimu wa 2022/23 ni muda wa kufanyia kazi ili kupunguza mateso kwa mashabiki pamoja na wachezaji katika kutimiza majukumu yao. Tunaona Mashujaa wamepanda wakiwaondoa Mbeya City kwenye mchezo wa mtoano lakini kuna baadhi…
MUDA wowote Yanga watatangaza kumuongezea mkataba wa miaka miwili kiungo wake mchezeshaji, Salum Aboubakari ‘Sure Boy’. Kiungo huyo alijiunga na Yanga katika msimu uliopita akitokea Azam FC ambayo ilivunja naye mkataba. Yanga imepanga kuiboresha safu hiyo ya kiungo kwa ajili ya msimu ujao ambao wanakwenda kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika. Taarifa zinaeleza kuwa Yanga wamefikia…
KLABU ya Simba imerudi tena ndani ya klabu ya Cotton Sports FC ya nchini Cameroon kwa ajili ya kuipata saini ya beki wa kati Che Fondoh Molane. Beki huyo ni kati ya wachezaji waliokuwa katika mipango ya kusajiliwa na Simba katika msimu huu katika kuiboresha safu ya ulinzi. Simba hivi karibuni ilitangaza kuachana na beki…
YANGA SC, imemtangaza Miguel Ángel Gamondi, kuwa kocha mpya wa timu hiyo akichukua mikoba ya Mtunisia, Nasreddine Nabi ambaye waliachana naye hivi karibuni baada ya mkataba wake kufikia tamati. Gamondi raia wa Argentina, anajiunga na Yanga akiwa mzoefu wa kufundisha soka Afrika kwa zaidi ya miaka 20, huku muda wake mwingi akiutumia kufundisha timu za…
BAADA ya mkataba wake kugota mwisho ndani ya kikosi cha Simba kipa Beno Kakolanya ameziingiza vitani Azam FC na Singida Big Stars ambayo kwa sasa inaitwa Singida Fountain Gate. Ni Singida Fountain Gate yenye maskani yake Singida hii inapewa nafasi kubwa kumnasa. Kipa huyo alikuwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania kilichopata ushindi…
CHUMA kipya Yanga hiki hapa, Simba yataja siku ya kumuaga Jonas Mkude ndani ya Spoti Xtra Jumanne
IMEKUWA ikitajwa kuwa mabosi wa Azam FC wapo kwenye mpango wa kuinasa saini ya Bernard Morrison. BM aliyekuwa kiungo wa Yanga raia wa Ghana kwa sasa yupo huru jambo lililowafanya viongozi wa klabu hiyo kuibuka na kuweka wazi kuwa nyota huyo hayuko kwenye mipango yao. Morrison alitangazwa kutokuwa kwenye mipango ya Yanga kwa msimu ujao…
STRAIKA Romelu Lukaku amegomea kujiunga na klabu za Saudi Arabia ambazo zimekuwa zikimwaga fedha nyingi kwa ajil ya kuzinasa saini za mastaa mbalimbali wa Ulaya. Lukaku ameongeza kuwa anataka kuendelea kubakia Ulaya kwa kuichezea timu ya Inter Milan ambayo yupo kwa mkopo akitokea Chelsea ambayo ilimsajili kutokea klabuni hapo. Klabu za Saudi Arabia zilikuwa zinamtaka…
AMEANDIKA Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba kuhusu Jonas Mkude ambaye hatakuwa katika kikosi hicho kwa msimu wa 2023/24 namna hii:- Ameondoka mtu tunaempenda kweli, ameondoka mtoto wetu, mtoto wa nyumbani kwetu. Kwa miaka ya hivi karibuni hakuna mchezaji tumewahi kumpenda kama Jonas Mkude na tutaendelea kumpenda. Wakati Simba ina njaa,…
WAITI mapesa wa Yanga afungukia usajili wa Manzoki Simba pamoja na usajili wa Aucho, Mayele
MSHAMBULIAJI wa Yanga Mkongomani Fiston Mayele ameibuka na kutamka kuwa tuzo tano alizozishinda msimu uliopita wa 2022/23 zimethibitisha ubora wake, huku akiwashukuru viongozi, wachezaji na mashabiki wa timu hiyo. Mshambuliaji huyo wa Yanga yupo Dar kwa sasa baada ya kuwa DR Congo alipokwenda katika majukumu ya timu ya taifa hilo, alikuwa kwenye kikosi kilichocheza dhidi…