VIDEO: JEMBE AFUNGUKIA KIPIMO CHA AZAM FC/ YANGA V SIMBA

LEGEND kwenye masuala ya michezo Bongo Saleh Ally Jembe ameweka wazi kuwa kwa mpira wa Tanzania ni ngumu kuwachambua wachezaji wa Bongo kwenye mechi za ndani kutokana na ushindani ambao upo na kila mmoja anatambua kufanya vizuri ni kwenye mechi za wenyewe kwa wenyewe.
Ni Yanga na Simba zilikuwa kwenye matamasha yao kwa ajili ya utambulisho wa wachezaji wapya kwa msimu wa 2023/24.

Amezungumzia kuhusu mchezaji bora kuwa Fiston Mayele wa Yanga, Dickson Job kuwa beki bora kutoka Yanga ambaye ni mzawa huku akibainisha kuwa hawana unafiki kwa wachezaji wanaofanya vibaya ikiwa ni pamoja na Kibu Dennis.