
KWAKO PILATO WA KARIAKOO DABI
TIMU zenye kiwango bora zaidi kwa Ukanda wa Afrika Mashariki kwa kipindi cha misimu saba sasa, ni Simba na Yanga. Simba imesumbua kwa muda mrefu, hasa kimataifa, wamekuwa wawakilishi wazuri wa Tanzania na Afrika Mashariki yote. Mwendo wa Simba, umefanya soka la Tanzania taratibu kupata heshima kubwa kimataifa na ile heshima waliyowahi kuwa nayo Ethiopia…