KAZI KUBWA IFANYIKE KWA KILA MMOJA

KAZI kubwa inafanyika kwa kila mmoja kuendelea na mapambano kusaka ushindi ndani ya uwanja. Muda ni sasa kuonyesha kwamba inawezekana kupata matokeo ugenini.

Benchi la ufundi tunaamini kwamba walipata muda wa kutosha kuzungumza na wachezaji. Sio kuzungumza pekee maneno ya kirafiki bali maneno ya kazi kuendelea kwa kila mmoja kutimiza majukumu yake.

Ukweli ni kwamba kazi ya kupeperusha bendera ya Tanzania kimataifa sio nyepesi. Muhimu kwa kila mmoja kufanya kazi yake kwa umakini ili kupata matokeo chanya.

Ni leo muda ambao timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia dhidi  Niger.

Ni kibarua kigumu ambacho Stars inabidi kupambana nacho kuhakikisha inapata matokeo. Dakika 90 zitaamua nini ambacho kitavunwa kwenye mchezo wa leo.

Mashabiki furaha yao ni kuona kazi inafanyika kwa wachezaji na matokeo yanapatikana. Kikubwa kwa watakaopewa kazi ya kuanza kikosi cha kwanza ni muda wa kufanya kweli kupata matokeo chanya.

Haitakuwa kazi rahisi lakini ukweli ni kwamba mchezo wa mpira ni mchezo wa makosa.Wachezaji wakipunguza makosa na kutumia nafasi watakazopata kuzibadili kuwa ushindi itaongeza nafasi kwao kusonga mbele kwenye mechi zijazo.

Baada ya mchezo dhidi ya Niger kazi nyingine itakuwa Uwanja wa Mkapa. Kwa mechi zote mbili muhimu kufanya kazi kubwa kupata ushindi.