Home Sports CHAMA MAMBO BADO MAGUMU KWAKE

CHAMA MAMBO BADO MAGUMU KWAKE

MWAMBA wa Lusaka, Clatous Chama mkali wa pasi za mwisho mambo bado ni magumu kwakwe kwa kushindwa kufurukuta kwenye mechi za hivi karibuni.

Ikumbukwe kwamba Oktoba 5 2023 ilikuwa ni mara ya mwisho kwa staa huyo wa Simba raia wa Zambia kufunga ndani ya ligi kwa msimu wa 2023/24.

Alifunga bao hilo kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons uliochezwa Uwanja wa Sokoine Mbeya walipokomba pointi tatu ugenini.

Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Tanzania Prisons 1-3 Simba. Kwenye mechi zilizofuata mwamba huyo aliganda kwa kushindwa kufunga wala kutoa pasi ya bao.

Ni shuhuda ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 1-5 Yanga katika Kariakoo Dabi iliyochezwa Novemba 5 akiwa yupo palepale na pasi yake moja.

Hata kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Namungo Uwanja wa Uhuru alianza kikosi cha kwanza alikwama kufunga wala kutoa pasi ya bao.

Msimu wa 2022/23 Chama alikuwa ni namba moja kwenye kutoa pasi za mwisho alipotoa pasi 14 za mabao upepo umekuwa mgumu msimu huu akiwa katoa pasi moja ya bao na kutupia mabao mawili.

Previous articleKAZI KUBWA IFANYIKE KWA KILA MMOJA
Next articleGerard Pique na Wengine 9 Sajili Zilizoshindwa kuonesha Maajabu Man Utd