MIKATABA YA WACHEZAJI IHESHIMIWE KUPISHANA NA KESI

    KESI nyingi ambazo zinawasumbua mabosi wengi wa timu ndani ya ardhi ya Tanzania ni kuhusu malipo. Mikataba ya wachezaji inakwenda kirafiki na hakuna ambaye anajali.

    Hili ni janga kubwa ambapo kila siku kumekuwa na kesi zinazowahusu wachezaji kufungua kesi kuhusu malipo yao. Haina maana kwamba waajiri hawatambui umuhimu wa kuwalipa hapana wanaamua kufanya makusudi.

    Mwisho wanaamua kuvunja mikataba na wachezaji bila ufuata utaratibu. Kesi zinakuwa nyingi kwa wachezaji kuamua kufungua kesi kuhusu malipo yao.

    Ikiwa itakuwa ni tabia kwa timu zote Bongo hili ni tatizo ambalo linahitaji kufanyiwa kazi kwa umakini. Hii itapunguza gharama ambazo zinazikumba timu husika kuwa kwenye sakata ya kulipa fedha baada ya wachezaji kushinda kesi zao.

    Muhimu kuzingatia makubaliano ya kwenye mikataba kwa viongozi kuwalipa wachezaji kwa wakati. Stahiki zao ni muhimu kufanyiwa kazi na wanapambana kutimiza majukumu yao wanapopata nafasi.

    Muda ni sasa kuendelea kutimiza majukumu ya kazi na kila mmoja atomize majukumu yake kwa wakati. Wachezaji wanakazi kubwa kwa sasa kuendelea kupambana kutimiza majukumu na viongozi wanapaswa kutimiza majukumu yao.

    Malipo kwa wakati na kuzingatia taratibu wakati wa kuvunja mikataba hilo litapunguza kesi ambazo zinapatikana mara kwa mara kwenye sekta ya michezo.

    Ikiwa wachezaji watalipwa kwa wakati basi itapunguza kesi nyingi kuripotiwa na wachezaji kufungua kesi kila wanapositishiwa mikataba yao na timu.

    Previous articlePICHA: TAIFA STARS YAONDOKA KWENDA MOROCCO KUKIWASHA NA NIGER MCHEZO WA KUFUZU KOMBE LA DUNIA
    Next articleNYOTA STARS WAAHIDI KUPAMBANA KIMATAIFA