SIO MUDA WA KUTAFUTA MCHAWI NANI NDANI YA TAIFA STARS

    MATUMAINI ya mashabiki wa Tanzania ni kuona kwamba wachezaji wanapata matokeo mazuri. Ipo hivyo hata wapambanaji wenyewe wanapoingia kwenye mapambano malengo ni kushinda.

    Mwisho matokeo ya mpira yanaptikana baada ya dakika 90. Kuna atakayeshinda na atakayeshindwa wakati mwingine inatokea wote wanatoshana nguvu kwenye mchezo husika.

    Kwa kilichotokea kwa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kupoteza mchezo dhidi ya Morocco ni sehemu ya mchezo. Makosa ya wachezaji uwanjani yamewaadhibu mwisho pointi tatu hazijabaki Tanzania.

    Ushindi ambao walipata Morocco iwe ni darasa lingine kwa mechi zijazo. Kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa ujezi hivyo kinachotakiwa ni kila mchezaji kujituma kusaka ushindi.

    Wachezaji wanatambua kwamba walipokosea hapo wapinzani wao walitumia kuwapa adhabu. Makosa yaliyotokea uwanjani ni maumivu kwa mashabiki na benchi la ufundi pia.

    Hivyo kwa mechi zinazofuata kwa ajili ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia ni muhimu kupambana uwapa furaha kwa mara nyingine mashabiki.

    Kete dhidi ya Niger ilichezwa vizuri na wachezaji wakapata ushindi. Furaha kubwa ilikuwa kwa wachezaji na mashabiki hivyo ni muda kwa ajili ya mechi zijazo kupambana kupata matokeo mazuri.

    Hakuna muda wa kuanza kumtafuta mchawi bali ni muda wa kufanyia kazi makosa ya mechi zilizopita. Inawezekana na kupata matokeo mazuri kwa mechi zijazo ambazo zitachezwa.

    Previous articleSIMBA AKILI KWA ASEC MIMOSAS ZIPO HIVI
    Next articleSIMBA WATUMA SALAMU HIZI KWA ASEC