VIWANJA VIBORESHWE LIGI IZIDI KUWA NA UBORA

    KILA leo tunashuhudia ligi yenye ushindani mkubwa kwa kila timu kuwa na mpango wa kuvuna pointi tatu kwenye mchezo husika.

    Katika mwendo wa ligi ambayo ushindani wake ni mkubwa tunaona kila timu inapambana kusaka ushindi na wale wanaotumia makosa ya wapinzani wanapata kile wanachostahili.

    Ushindani umekuwa mkubwa na hali hii inatakiwa kuwa endelevu mpaka mwisho wa msimu ili kufanya kila mchezaji aone thamani ya kushiriki ligi na kucheza kwa kujituma.

    Kwa wachezaji nao wana kazi ya kuonyesha kile ambacho wanacho kwenye miguu yao kwa kucheza kwa akili pamoja na nidhamu ili kutimiza malengo yao pamoja na ya timu kiujumla.

    Sio kazi rahisi kufikia malengo ikiwa wachezaji watashindwa kutimiza majukumu yao kwa umakini.

    Ipo wazi kwamba mwanzo kila timu huwa inakuwa na shauku ya kuonyesha kile ilicho nacho. Kwa kufanya hivyo kunaongeza ushindani na nguvu ya kila mchezaji kusaka ushindi ndani ya uwanja.

    Mwendo ambao unakwenda kwa sasa ni msako wa pointi na hakuna timu ambayo haipendi kushinda hivyo mashabiki nao wanapswa kuendelea kuwa pamoja  na timu zao bila kukata tamaa.

    Nina amini kwamba kila timu imeweka mpango kazi kwa ajili ya kufikia malengo yake. Ili kufikia malengo ni lazima kila mmoja awe ndani ya timu jambo hili litasaidia kufanikisha mipango kwa wakati.

    Tukiachana na hayo sasa hebu tutazame sehemu muhimu ambayo inahusika kutoa ushindi kwa wachezaji wawapo kazini kusaka pointi tatu ambapo ni ndani ya uwanja.

    Ubora wa uwanja hasa sehemu ya kuchezea ni muhimu kuwa bora wakati wote ili kutoa burudani kwa wale ambao wanacheza pamoja na mashabiki ambao wanajitokeza kuona burudani.

    Ukweli ni kwamba wengi huwa wanatazama sehemu ya kukaa mashabiki pamoja na sehemu ya kubadilishia nguo na kuachana na habari za sehemu ya kuchezea.

    Kuna mashindano mengi ambayo yanaendelea kwa sasa ni muhimu kwa sehemu ya kuchezea kuwa bora na kutunzwa ili iweze kuwa rafiki kwa wachezaji pamoja na kutoa matokeo mazuri ndani ya uwanja.

    Kuna baadhi ya viwanja ambavyo vilifungiwa kutokana na kutokidhi vigezo hivyo ni muhimu kwa wahusika kulitazama kwa ukaribu. Wale ambao bado hawajafungiwa ni muhimu kufanyia maboresho kwenye viwanja husika.

    Muhimu kuwa na sehemu nzuri ya kuchezea ili kuwapa nafasi wachezaji kuonyesha ule uwezo wao kwa kuwa imekuwa ni tatizo la muda wote hasa kwenye suala la viwanja bado mambo yamekuwa ni magumu.

    Matokeo ndani ya uwanja yanapatikana ikiwa sehemu ya kuchezea itakuwa bora na kila mmoja atacheza kwa kujiamini tofauti na viwanja vingine ambavyo havikuwa bora.

     Ikiwa viwanja vingine vipo na havina ubora ninashauri  vifanyiwe maboresho na yakitokea haya mafanikio makubwa yataonekana hapo baadaye.

    Maboresho ya sehemu ya kuchezea yaendane pia na sehemu ya kubadilishia nguo hilo nalo ni la msingi litafanya ushindani uzidi kuwa mkubwa wakati wote.

    Wale ambao watakuwa wanakaa eneo la mashabiki ikiwa ni sehemu nzuri watafurahi kuona mpira mzuri kutoka kwa wachezaji wakiwa uwanjani.

    Wachezaji nao wakiwa wanacheza kwenye uwanja mzuri inaongeza nguvu kwa wao kupambana kwa juhudi kubwa kusaka ushindi wa timu katika mazingira ambayo wanayapenda.

    Mpira ni burudani na kila mmoja anapenda kuona namna pasi zikipigwa na ushindi ukipatikana baada ya dakika 90 hivyo muhimu kufanya maboresho kwa wakati huu uliopo.

    Kikubwa kinachotakiwa katika hili ni kuona kwamba kila mmoja anaweza kufikia malengo lakini asiwepo yule wa kumrudisha nyuma mwingine lazima uwajibikaji uendelee ndani ya kile ambacho wanakifanya.

    Previous articleMERIDIANBET YAINEEMESHA MWENGE WAGAWA MIAMVULI
    Next articleFT: Machester United 0-3 Bournemouth