
POLISI TANZANIA V COASTAL UNION NI LEO
MKALI wa kucheka na nyavu ndani ya Ligi Kuu Bara,Vitalis Mayanga akiwa na mabao manne ametuma ujumbe kwa Coastal Union kuwa wanahitaji pointi tatu. Timu hizo zinatarajiwa kukutana leo Novemba 19 katika Uwanja wa Ushirika,Moshi mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Mayanga amesema kuwa mechi zao zote ambazo watacheza wanahitaji ushindi ili waweze kufikia malengo…