FOUNTAIN GATE:MWENDO WA CHAMPIONSHIP ACHA TU

KIUNGO wa Fountain Gate,Daud Rashid ameweka wazi kuwa moto wa Championship sio wa kitoto kwa kuwa kila timu inapambana kusaka pointi tatu uwanjani.

Kwenye msimamo timu hiyo ipo nafasi ya 6 baada ya kucheza mechi 7 kibindoni ina pointi 12 huku vinara wakiwa ni DTB FC wenye pointi 17.

Rashid amesema kuwa hakuna timu ya kubeza kwenye ligi jambo ambalo linaongeza ugumu kwenye kupata matokeo.

“Kwa sasa tunacheza mfumo wa ligi sasa kila timu ambayo unakutana nayo imejipanga kupata pointi tatu hapo lazima mambo yawe magumu kwa kila timu kusaka ushindi lakini hilo ni jambo jema kwa kuwa ili ligi iwe bora ushindani ni lazima.

“Yote kwa yote bado tunazidi kupambana ili kupata matokeo kwa kuwa malengo yetu ni kuona tunapata pointi tatu na hilo linawezekana, mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,” amesema Rashid.

Novemba 20, Fountain Gate itakuwa na mchezo dhidi ya Ihefu FC katika mwendelezo wa Championship utachezwa Uwanja wa Highland Estate,Mbeya.