>

AJIBU AONDOLEWA KIKOSINI SIMBA NA MUGALU

NYOTA wawili wa kikosi cha Simba Ibrahim Ajibu na Chris Mgalu wameondolewa kwenye kikosi hicho kinachojiaandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting.

Leo Novemba 19, Pablo Franco anatarajia kukiongoza kikosi hicho kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting unaotarajiwa kuchezwa saa 10:00 jioni, Uwanja wa CCM Kirumba.

Sababu za nyota hao kuondolewa kikosini ni kusumbuliwa na majeraha jambo ambalo linawafanya wasiwe tayari kuwa kwenye kikosi cha kwanza dhidi ya Ruvu Shooting leo.

Ajibu kwenye mazoezi ya Novemba 16, Uwanja wa Boko Veteran alikuwa chini ya uangalizi maalumu kwa kuwa hakuwa fiti baada ya kupata majeraha kwenye mguu wake wa kulia.

Kwa upande wa Mugalu yeye hakuwepo mazoezini kwa kuwa alikuwa akitibu majeraha yake baada ya kujitonesha alipokuwa akicheza mbele ya Dodoma Jiji ila kwa sasa anaendelea vizuri.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu amesema kuwa Ajibu aliumia mazoezini baada ya kujikwaa Uwanja wa Boko Veteran.