>

DIARRA KUMPA CHANGAMOTO AISHI MANULA

MILTON Nienov aliyekuwa kocha wa makipa ndani ya Simba ameweka wazi kuwa kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula atapata changamoto kubwa kutoka kwa kipa wa Yanga,Diarra Djigui.

Nienov kwa sasa ameshachimbishwa ndani ya Simba ilikuwa ni Septemba 26 kwa kile kilichoelezwa ni makubaliano ya pande zote mbili.

Nienov aliweka wazi kwamba anatambua ubora wa Manula kwa kuwa alikuwa akimfundisha ila kuna ugumu ataupata msimu huu kutoka kwa Diarra.

“Ukitaja makipa bora kwa sasa ndani ya ligi huwezi kuliacha jina la Manula kwa kuwa nimemfundisha na ninamtamubua lakini kwa namna ambavyo mabo yanakwenda kwa sasa kuna ugumu ataupata kutoka kwa Diarra.

“Nilipata muda wa kumtazama na nilimuona kwenye mechi kubwa namna ambavyo alikuwa akifanya naona wazi kwamba atampa wakati mgumu Manula ambaye najua hatakubali kushindwa hivyo anapaswa kupambana bila kuchoka,” alisema.

Kwa msimu wa 2021/22 makipa wote wametumia dakika 450 kwenye mechi tano, Manula hajafungwa kwenye mechi zote hizo tano huku Diarra akifungwa kwenye mechi moja na mechi nne hajafungwa.