POLISI TANZANIA V COASTAL UNION NI LEO

MKALI wa kucheka na nyavu ndani ya Ligi Kuu Bara,Vitalis Mayanga akiwa na mabao manne ametuma ujumbe kwa Coastal Union kuwa wanahitaji pointi tatu.

Timu hizo zinatarajiwa kukutana leo Novemba 19 katika Uwanja wa Ushirika,Moshi mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Mayanga amesema kuwa mechi zao zote ambazo watacheza wanahitaji ushindi ili waweze kufikia malengo ambayo wamejiwekea.

“Malengo yetu ni kupata ushindi kwenye mechi zetu ambazo tutacheza na hilo linawezekana kutokana na kila mchezaji kuhitaji kuona matokeo hivyo kila mchezo kwetu tunauchukulia kwa uzito mkubwa,” amesema Mayanga.

Mayanga mbali na kufunga mabao hayo manne kwenye mechi tano pia ana pasi moja ya bao huku akifanya kazi na mkongwe Kelvin Yondan ambaye ni nadhodha wa timu na kipa wao namba moja na kipa wao namba moja ni Metacha Mnata.

Kwa upande wa staa wa Coastal Union, Hance Masoud ambaye amefunga bao moja na pekee kwa Coastal Union amesema kuwa wapo tayari kwa ushindani.