Home Sports GADIEL MICHAEL:TUNAWAHESHIMU RUVU SHOOTING,TUPO TAYARI

GADIEL MICHAEL:TUNAWAHESHIMU RUVU SHOOTING,TUPO TAYARI

BEKI wa Simba, Gadiel Michael amesema kuwa kuelekea mchezo wa leo wa Ligi Kuu Bara dhidiya Ruvu Shooting kutakuwa na mabadiliko kwa kuwa wachezaji wapo tayari licha ya ushindani kuwa mkubwa.

Gadiel bado hajacheza ndani ya msimu wa 2021/22 kwa sasa katika mechi tano na nafas yake amekuwa akianza nyota Mohamed Hussein ambaye ni chaguo la kwanza ndani ya kikosi hicho.

Leo Simba ina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Ruvu Shooting kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Beki huyo amesema:”Tunawaheshimu Ruvu Shooting na tunajua kwamba mchezo wetu hautakuwa rahisi lakini tupo tayari kwa ajili ya kuweza kupata ushindi.

“Mashabiki wawepamoja nasi kwani tayari kuna mabadiliko ambayo yapo na uwepo wa mwalimu mpya pia ni jambo ambalo linatufanya nasi tuwe kwenye hesabu nyingine.

“Mwendo ambao tumeanza nao tunajua kwamba haujawa wa kufurahisha lakini kuna maendeleo ambayo yanahitajika kuonekana hivyo kwenye mchezo wetu dhidi ya Ruvu Shooting ni muhimu mashabiki kuwa nasi bega kwa bega,” .

Previous articlePOLISI TANZANIA V COASTAL UNION NI LEO
Next articleKHALID AUCHO KUIKOSA NAMUNGO KESHO