INIESTA NA MESSI WATAJWA BARCELONA

JOAN Laporta, rais wa Barcelona amebainisha kuwa jambo lolote linaweza kutokea kuhusu suala la Lionel Messi pamoja na Andre’s Iniesta kurejea ndani ya Camp Nou.

 

Tayari Barcelona inayoshiriki La Liga imemrejesha staa wao wa zamani beki wa makombe Dani Alves ambaye alikuwa ni chaguo la Kocha Mkuu, Xavi Hernandez.

Alves mwenye miaka 38 amesaini dili la muda mfupi hadi mwishoni mwa msimu huu na alitambulishwa mbele ya mashabiki 10,000 wa timu hiyo kwenye Uwanja wa Camp Nou.

Messi mwenye miaka 34 aliondoka bure ndani ya Barcelona na kuibukia PSG huku Iniesta mwenye miaka 37 yupo zake ndani ya Klabu ya Vissel Kobe ya Japan tangu 2018.

Rais amesema kuwa hawezi kusema kama wanaweza kurudi ama la ila lililotokea kwa Dani Alves linaweza kumpata mwingine.