
MASTAA YANGA WAIPIGA MKWARA BIASHARA UNITED
MASTAA wa Yanga wameweka wazi kuwa watakachowafanyia Biashara United ni kuchukua pointi zao tatu kwa ajili ya kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa msimu huu. Yanga kwa sasa ni vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa wamejikusanyia jumla ya alama 23 mara baada ya kushinda michezo saba na kutoa sare miwili katika michezo tisa ambayo wamecheza mpaka sasa. Yanga leo Jumapili Desemba 26, wanatarajiwa kumenyana na Biashara United katika mchezo unaotarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar….