
KAZI KIMATAIFA LEO HAKUNA MWENYE SHUGHULI NDOGO
HATIMAYE imefika siku ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki pamoja na benchi la ufundi kuona kipi kitapatikana ndani ya dakika 90. Ligi ya Mabingwa Afrika, mashindano yenye ushindani mkubwa yanatarajiwa kuendelea leo na wawakilishi wa Tanzania, Simba na Yanga watakuwa kazini. Yanga watakuwa nyumbani Uwanja wa Mkapa huku Simba wakiwa ugenini, Botswana wote…