UGUMU WA NAMBA UMEONGEZEKA YANGA SABABU HII HAPA

UWEPO wa nyota wapya ndani ya kikosi cha Yanga unatajwa kuwa sababu ya kuongeza ugumu wa namba kwenye kikosi hicho kinachofundishwa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi raia wa Algeria. Miongoni mwa wachezaji wapya waliongezwa ni mshambuliaji mmoja, kiungo mshambuliaji pamoja na mkabaji kwenye dirisha dogo la usajili.