Home Sports SINGIDA FOUNTAIN GATE NA SABABU ZA KUUZA WACHEZAJI

SINGIDA FOUNTAIN GATE NA SABABU ZA KUUZA WACHEZAJI

UONGOZI wa Singida Fountain Gate umeweka wazi kuwa sababu kubwa ya kufanya biashara ya kuwauza wachezaji wao waliokuwa na uhakika wa namba kikosi cha kwanza ni kupata fedha za kulipa madeni.

Timu hiyo ipo ndani ya tano bora na imekuwa ikileta ushindani mkubwa kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara kutokana na mipango makini kwenye kusaka ushindi.
Kwenye Mapinduzi 2024 waligotea hatua ya nusu fainali kwa kuondolewa na Simba kwenye hatua ya penalti ambapo katika hatua ya robo fainali waliwaondoa wababe Azam FC.
Rais wa Singida Fountain Gate, Joseph Makau amesema kuwa wanatambua umuhimu wa kuwa na wachezaji wazuri na walifanya biashara na timu ili kupata fedha kwa ajili ya kulipa madeni.
“Ni kweli tumeuza baadhi ya wachezaji wetu ili kupata fedha za kulipa madeni ya klabu. Kuna timu ambazo zilikuja kwa ajili ya kupata wachezaji wetu tulikaa nao mezani na tulishindwana kwenye bei,” amesema.
Miongoni mwa wachezaji ambao hawatakuwa kwenye kikosi hicho ni Meddie Kagere ambaye yupo Namungo, Gadiel Michael ambaye atakuwa Cape Town.

Previous articleUGUMU WA NAMBA UMEONGEZEKA YANGA SABABU HII HAPA
Next articleCHEZA SLOTI YA FASHION NIGHT USHINDI X500