PICHA LA YANGA KUCHUKUA UBINGWA WA LIGI LIMECHORWA HIVI
MTENDAJI Mkuu wa Yanga, Senzo Mbatha Mazingiza, ameweka wazi mpango mkakati wa kuhakikishatimu yao inatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu ni kuuchukulia kila mchezo kama fainali jambo ambalo litawanufaisha zaidi kukusanya pointi katika michezo yao. Yanga mpaka sasa wanaongoza ligi kuu wakiwa na pointi 15 baada ya kufanikiwa kushinda michezo yote mitano, wakiwa wamefunga mabao tisa na kuruhusu moja. Senzo amesema ukubwa wa Yanga ndio chanzo cha kuhitaji kutwaa ubingwa…