>

PICHA LA YANGA KUCHUKUA UBINGWA WA LIGI LIMECHORWA HIVI

MTENDAJI Mkuu wa Yanga, Senzo Mbatha Mazingiza, ameweka wazi mpango mkakati wa kuhakikisha
timu yao inatwaa ubingwa 
wa Ligi Kuu Bara msimu huu ni kuuchukulia kila mchezo kama fainali jambo ambalo litawanufaisha zaidi kukusanya pointi katika michezo yao.


Yanga mpaka sasa 
wanaongoza ligi kuu wakiwa na pointi 15 baada ya kufanikiwa kushinda michezo yote mitano, wakiwa wamefunga mabao tisa na kuruhusu moja.

 

Senzo amesema ukubwa wa Yanga ndio chanzo cha kuhitaji kutwaa ubingwa katika kila msimu, huku akiweka wazi msimu huu wanatakiwa kuchukulia kila mchezo kama fainali jambo ambalo litasababisha kufikia malengo mapema tu.

“Tumeanza msimu vizuri kwa kukusanya pointi nyingi, hiyo ni kutokana na kupambana katika kila mchezo, siri kubwa ya kukusanya pointi nyingi msimu huu ni kuchukulia kama fainali katika kila mchezo.

 

“Baada ya hapo basi tutashinda michezo mingi na kukusanya pointi za kutosha ambazo zitatufanya tuweze kuwa mabingwa msimu huu mapema tu.

“Msimu huu timu nyingi zimejipanga na ligi ni ngumu, hivyo kama tutakuwa tunadharau mchezo kwa kusema ni mrahisi basi hatutafikia malengo yetu.

“Viongozi, wachezaji na benchi la ufundi wote wanafahamu hili na wote kwa pamoja tupo tayari kwa ajili ya utekelezaji,” alisema kiongozi huyo.