>

KAGERE ATUPIA MABAO 60 BONGO

MEDDIE Kagere ndani ya kikosi cha Simba kwa msimu wa 2021/22 ameshindikana kwa kuwa ni kinara wa mabao akiwa nayo mawili na amefunga yote akitokea benchi na kumfanya afikishe jumla ya mabao 60 ndani ya Ligi Kuu Bara tangu aanze kucheza Bongo.


Kagere aliyeibuka ndani 
ya Simba msimu wa 2018/19, bao lake la kwanza kwa msimu wa 2021/22 alipachika mbele ya Dodoma Jiji akitumia pasi ya mshikaji wake Chris Mugalu na alifunga akitoka benchi.


Mabao yake 60 kwa sasa 
yanatokana na uwepo ya yale aliyofunga msimu wake wa kwanza ambayo ni 23 na Simba
ilifunga jumla ya mabao 77 
baada ya kucheza mechi 38.


Mabao yake mengine ni yale 
aliyotupia msimu wa 2019/20 akiweka kambani 22 na alikuwa ni namba moja kwa utupiaji. Msimu wa 2020/21 Kagere alitupia mabao 13.

 

Simba ikiwa inapata tabu kwenye eneo la ushambuliaji, Kagere ametupia mabao mawili na kumfanya aweze kufikisha jumla ya mabao 60 akiwa ana kazi ya kuifukuzia rekodi ya mzawa John Bocco ambaye ni mfungaji bora wa muda wote akiwa ametupia mabao zaidi ya 100 Bongo.