>

ISHU YA YANGA KUBADILI NEMBO YA MDHAMINI YATOLEWA UFAFANUZI

MKURUGENZI wa Bodi ya Ligi, Almasi Kasongo ametoa ufafanuzi kuhusu baadhi ya vilabu vya soka nchini kubadili nembo za wadhamini kwenye jezi zao.

Nembo ya mdhamini wa Ligi Kuu Bara NBC ina rangi nyekundu jambo ambalo halikubaliki kwa Yanga kwa mujibu wa katiba yao jambo ambalo limepelekea wao kubadilishiwa nembo na kuvaa twiga mwenye rangi nyeusi.

“Suala la nembo ni suala la kikanuni na bodi ya ligi kazi yake kusimamia kanuni mwenye dhamana ya kusimamia hilo ni yule mwenye nembo yake.

 

“Bodi ya ligi inanembo yao TFF ina nembo yao na kila klabu ina nembo yake. Bodi tutasimamia kanuni zinavyosema na pia tutazingatia makubaliano baina ya mwenye nembo na klabu husika.

 

“Na haiwezekani mwenye nembo aseme tumekubaliana na mhusika flani halafu bodi ipinge, bodi ipo kwa ajili ya kusave interest ya klabu na bodi ya ligi ni sulihisho na si kuwa chanzo cha tatizo kwa wadau wetu,” CEO TPLB Almasi Kasongo akitolea ufafanuzi kwanini wamekubali Yanga SC kuvaa twiga mweusi.