Home Sports DTB YASEPA NA POINTI TATU MBELE YA KEN GOLD

DTB YASEPA NA POINTI TATU MBELE YA KEN GOLD

RAMADHAN Nswazurimo, Kocha Mkuu wa Klabu ya DTB amesema kuwa wachezaji wake waliamini wameshinda kwenye mchezo wa leo dhidi ya Ken Gold jambo lililowafanya wapate tabu ndani ya dakika 90.

 

Mchezo wa leo wa Championship uliochezwa Uwanja wa Uhuru ulikuwa na ushindani mkubwa na timu zote zilikuwa zikishambuliana kwa zamu.

Mwisho wa siku ushindi umekuwa mali ya DTB baada ya kushinda kwa mabao 2-1 na bao la ushindi lilipachikwa na nyota wao James Msuva ambaye alimaliza utata na kuipa pointi tatu timu hiyo.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo Nswazurimo amesema kuwa kipindi cha kwanza wachezaji wake walikuwa wakicheza kwa kujifurahisha wakiamini wamemaliza kazi.

“Wachezaji kipindi cha kwanza walikuwa wakicheza kwa kujifurahisha walikuwa wanaamini kazi imekwisha ila mwisho wa siku niliwaambia waongeze umakini wapinzani wetu wapo imara.

“Kwa kuwa tumeshinda basi hilo ni jambo la furaha kwetu sasa acha tupate muda wa kupumzika kushangilia ushindi wetu,”

Previous articleKAGERE ATUPIA MABAO 60 BONGO
Next articleTAIFA STARS WAENDELEA KUIVUTIA KASI DR CONGO