Home Sports TAIFA STARS WAENDELEA KUIVUTIA KASI DR CONGO

TAIFA STARS WAENDELEA KUIVUTIA KASI DR CONGO

KIKOSI cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo Novemba 7 kimeendelea na mazoezi kwa ajili ya mechi za kimataifa za kufuzu Kombe la Dunia.

Mchezo ujao kwa Stars ni dhidi ya DR Congo ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa unasubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki wa soka Bongo.

Utachezwa Novemba 11,2021, Uwanja wa Mkapa saa 10:00 jioni kwa timu zote mbili zitakapokuwa uwanjani kusaka ushindi.

Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amesema kuwa anaamini kwamba timu hiyo itapata matokeo chanya mbele ya DR Congo, kwenye mchezo huo.

“Wachezaji wanajua kwamba tunahitaji ushindi na morali ni kubwa hivyo imani yetu ni kuona kwamba tunapata matokeo na tunaweza kufuzu Kombe la Dunia licha ya kwamba haitakuwa rahisi,”.

Kwenye kundi J Stars inaongoza kundi ikiwa na pointi 7 sawa na Benin inafuatiwa na DR Congo kisha wanafunga nafasi ya nne ni Madagascar.

Previous articleDTB YASEPA NA POINTI TATU MBELE YA KEN GOLD
Next articleKUFURU TUPU KOCHA SIMBA,NABI AVUNJA KIKOSI YANGA,NI CHAMPIONI JUMATATU