KLABU ya Yanga imepigwa faini ya shilingi laki tano kwa kosa la kuwakilishwa na maofisa wanne badala ya watano katika kikao cha maandalizi ya mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Mkapa.
Mkutano huo kwa mujibu wa taarifa imeeleza kuwa ulifanyika Novemba 2, Uwanja wa Mkapa.
Adhabu hiyo imetolewa kwa kwa uzingativu wa kanuni ya 17,(2) na 17,(60) ya Ligi Kuu Bara Tanzania kuhusu taratibu za michezo.
Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara,(TPLB) katika kikao chake cha Novemba 5,2021.