>

KUMBE! SIMBA WANAITAKA TIMU NZIMA YA YANGA

MAKAMU Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Klabu ya YANGA, Eng Hersi Said amesema amepata tetesi za viongozi wa klabu ya Simba hivi karibuni kuonekana mara kadhaa nyumbani kwa wazazi wa beki kinda wa Yanga Kibwana Shomari.

 

“Ninazo taarifa hizo kupitia mchezaji mwenyewe na watu wangu wa karibu kuhusu ziara zenye nia ya kumshawishi beki wetu kijana ili ajiunge nao, Lakini nikwambie tu sisi kama Yanga tupo kisasa mno siku hizi hizo mbinu zao ni za kizamani  kama wanaume kweli waje mezani walete mzigo, huo ujanja ujanja wao hautawasaidia kamwe.

 

“Siyo Kibwana tu ambaye wanamnyatia tunazo taarifa nyingi kuhusu wachezaji wetu karibia ‘back line’ yetu yote wanaitaka, halafu kiungo chetu chote wanakitaka winga zetu wanazitaka. Sasa sijui wana hela kiasi gani  na mimi siwashangai hawana ‘scouting’ nzuri ya kutafuta wachezaji.

 

“Timu waliyonayo inaitwa asante Azam, sababu wachezaji wote waliotamba nao miaka mitatu iliyopita walipewa kama sadaka na Azam,” alisema Eng. Hersi.