
BEKI WA KAZI KUSAJILIWA YANGA KUONGEZA NGUVU KWA JOB
UONGOZI wa Yanga umefunguka kuwa kuna uwezekano mkubwa wakaingia sokoni na kusajili beki mmoja wa kati mwenye uwezo mkubwa ili kuwa msaada kwa Dickson Job na Bakari Mwamnyeto ambao ndiyo tegemeo kwa sasa. Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Thabiti Kandoro alipokuwa anaweka wazimipango ya timu hiyo kwenye dirisha dogo la usajili ambalo limefunguliwa Desemba 16,mwaka huu na kutarajiwa kufungwa Januari 15, mwakani. Akizungumza na Spoti Xtra, Kandoro alisema viongozi wametazama kikosi na kupitia…