Home Sports BABA SURE BOY AFUNGUKIA ISHU YA MWANAE KUCHEZA YANGA

BABA SURE BOY AFUNGUKIA ISHU YA MWANAE KUCHEZA YANGA

BABA mzazi wa kiungo wa Azam FC, Salum Aboubakar ‘Sure Boy’, mzee Aboubakar Salum ‘Sure Boy Sr’ ameweka
wazi kuwa mtoto wake yupo 
mbioni kumalizana na mabosi wa Yanga baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuvunja mkataba wa mchezaji huyo na Azam FC kutokana na mgogoro uliokuwepo.


Kiungo huyo ni miongoni mwa 
wachezaji watatu wa Azam FC waliosimamishwa kwa utovu wa
nidhamu. Wengine ni Agrey Morris 
na Mudathir Yahya.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, mzee Aboubakar alisema mtoto wake amebakisha asilimia chache za kujiunga na Yanga baada ya kufikia makubaliano kwenye mambo mengi ya msingi huku akienda mbali akisema tayari mkataba wake na Azam umeshavunjwa na TFF.


“Nilianza kusikia kwenye 
vyombo vya habari lakini tayari kijana mwenyewe amenieleza kila kitu juu ya Yanga, tayari wameshakubaliana vitu vingi na mabosi wa Yanga kwa ajili ya kusaini mkataba baada ya TFF kuuvunja mkataba wake na Azam kutokana na mgogoro wao wa muda mrefu.


“Nadhani kwa sasa watakuwa 
wamebakisha mambo machache ya kimasilahi kabla ya kumalizana kabisa, suala ya yeye kwenda kwenye timu ambayo nilicheza kwangu ni jambo zuri japokuwa sikutaka iwe hivyo, ila kutokana na
matatizo yake na Azam imekuwa ni 
jambo kubwa.


“Yanga kuna wachezaji wengi 
wazuri, suala la yeye kucheza itategemea na mwalimu atatumia mfumo gani, ila naamini atacheza tu,” alisema Sure Boy Sr.

Previous articleTANZANIA YATWAA MAKOMBE 7,MAJALIWA ATOA SALAMU ZA PONGEZI
Next articleROBO FAINALI YA CARABAO CUP KUCHEZWA WIKI HII