BABA SURE BOY AFUNGUKIA ISHU YA MWANAE KUCHEZA YANGA
BABA mzazi wa kiungo wa Azam FC, Salum Aboubakar ‘Sure Boy’, mzee Aboubakar Salum ‘Sure Boy Sr’ amewekawazi kuwa mtoto wake yupo mbioni kumalizana na mabosi wa Yanga baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuvunja mkataba wa mchezaji huyo na Azam FC kutokana na mgogoro uliokuwepo. Kiungo huyo ni miongoni mwa wachezaji watatu wa Azam FC waliosimamishwa kwa utovu wanidhamu. Wengine ni Agrey Morris na Mudathir Yahya. …