Home International RUDIGER KUKUNJA MKWANJA MREFU REAL MADRID

RUDIGER KUKUNJA MKWANJA MREFU REAL MADRID

IKIWA dili lake litakamilika kujiunga na kikosi cha Real Madrid akitokea Klabu ya Chelsea basi beki Antonio Rudiger atakunja mkwanja mrefu kweli.

Rudiger anatarajiwa kuondoka kwenye kikosi hicho na timu kadhaa Ulaya zinatajwa kuwania saini yake.

Ambao wapo mbele kuwania saini ya mwamba huyo ni Real Madrid ambao wao wametenga kabisa kitita cha mshahara wa pauni 400,000 kwa wiki.

Ni mara ya pili tayari Madrid wamepeleka ofa kwa ajili ya kumpata beki huyo lakini wamekutana na kizingiti kutoka kwa PSG na Bayern Munich ambao nao pia wanawania saini ya beki huyo.

Beki hyuyo mwenye miaka 28 mkataba wake ndani ya Chelsea umebakiza miezi sita na Chelsea nao pia wanahitaji huduma ya kitasa hicho.

Previous articleMAJEMBE MAPYA YANGA KUANZA KAZI
Next articleTANZANIA YATWAA MAKOMBE 7,MAJALIWA ATOA SALAMU ZA PONGEZI