Rekodi za Namungo FC 1-3 Yanga SC NBC Premier League

Mabingwa watetezi wa NBC Premier League, Yanga SC chini ya Kocha Mkuu, Manqoba Mngqithi wamefungua ukurasa wa kwanza kwa kushuhudia ubao wa Uwanja wa Majaliwa, Agosti 15,2026 ukisoma Namungo FC 1-3 Yanga SC.

Weka kando matokeo hayo ya ushindi kwa wageni, dakika 90 zilitawaliwa na rekodi kibao ambazo zimeandikwa na hapa tunakuletea 5 ambazo zilibamba namna hii:-

Bao la Namungo FC pasua kichwa

Herbet Lukindo, mfungaji wa bao la kwanza ndani ya Namungo FC ni pasua kichwa kwa namna alivyowavuruga mabeki wat imu pinzani. Wakati mabeki wakiamini yupo kwenye mtego wa kuotea bado alijiamini na kuhakikisha mpira unazama kimiani dakika ya 76.

Lukindo anakuwa mchezaji wa kwanza kumtungua kipa namba moja wa Yanga SC, Djigui Diarra ndani ya NBC Premier League 2026/27.

Boka mfungaji wa bao la kwanza Yanga SC

Chadrack Boka beki wa Yanga SC anaingia kwenye rekodi ya kuwa mfungaji wa bao la kwanza ndani ya 2026/27. Beki huyo ilibidi asubiri mpaka dakika ya 68 kufunga bao hilo mara baada ya kipa kupishana na mpira aliokuwa akitaka kuokoa.

Baada ya bao hilo zilipita dakika 2, Maxi Nzengelin aye akafungua akaunti ya mabao akifunga kamba ya pili katika mchezo huo ulioshuhudia dakika 45 za mwanzo zikikamilika bila nyavu kutikishwa.

VAR imeanza kazi

Teknolojia imeanza kazi kwenye NBC Premier League kupunguza yale makosa ya kibinadamu. Pongezi kwa waamuzi kuanza na mwendo makini. Dakika ya 58 kulikuwa na maamuzi ya kuotea baada ya Yanga SC kufanya shambulizi kwa Namungo FC.

Majadiliano na marejeo yalionyesha kuwa maamuzi ya mwanzo yalikuwa sahihi, hivyo Yanga SC hawakupewa bao. Dakika ya 68, Herbet Lukindo wa Namungo FC alipofunga bao benchi la ufundi la Yanga SC maamuzi yalikubali ni bao hata marejeo majibu yalikuwa ni bao.

Namungo FC hawana bahati na Yanga SC

Mchezo wa Agosti 15,2026 unakuwa ni mchezo wa 15 kwa wababe hawa kukutana na Yanga SC. Katika mechi hizo hawajapata ushindi mbele ya watoto wa Jangwani. Yanga SC imepata ushindi mara 10, sare ikiwa ni mechi 5. Kwenye dakika 1,350 ambazo wamekutana yamefungwa jumla ya mabao 36, Yanga SC imefunga mabao 27 Namungo FC mabao 9.

Maxi Nzengeli aanza na tuzo

Mpaka dakika 90 zinakamilika nyavu zilitikiswa jumla ya mabao 4. Miongoni mwa waliofunga ni kiungo Maxi Nzengeli aliyepachika bao dakika ya 70 akiwa nje ya 18.

Nzengeli anaandika rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kusepa na tuzo ya mchezaji bora kwenye mechi ya kwanza ndani ya kikosi cha Yanga SC, 2026/27. Kituo kinachofuata kwa Yanga SC ni Agosti 20,2026 dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa Uhuru, Dar.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.

Duniani kote kinapatikana mtandaoni bofya hapa Buy Book: Msichana wa Maisha Yangu by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar.