Home Sports SURE BOY APEWA MIAKA MIWILI YANGA

SURE BOY APEWA MIAKA MIWILI YANGA

RASMI kiungo mchezeshaji wa Azam FC, Salum Aboubakari ‘Sure Boy’ amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga.


Hiyo ikiwa ni siku chache 
tangu usajili wa dirisha dogo ufunguliwe Desemba 16, mwaka huu. Huyo anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Yanga baada ya hivi karibuni kumsaini kiungo mshambuliaji wa Biashara United, Denis Nkane.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo limezipata Spoti Xtra, kiungo huyo alisaini mkataba huo baada ya kuvunja mkataba wake na Azam FC.

Mtoa taarifa huyo alisema, Sure Boy hivi karibuni atajiunga na Yanga kwa ajili ya kuanza mazoezi ya pamoja na wenzake.


“Sure Boy ni mali ya 
Yanga baada ya wiki moja iliyopita kusaini mkataba wa miaka miwili baada ya kufikia makubaliano mazuri.


“Azam wamekubali 
kumuachia baada ya mchezaji mwenyewe kuomba kuondoka,” alisema mtoa taarifa huyo.


Makamu Mwenyekiti 
wa Yanga, Frederick Mwakalebela, alizungumzia hilo kwa kusema: “Kila kitu kinachohusiana na usajili kipo kwa kocha Nabi (Nasreddine) ambaye ndiye anapendekeza usajili, hivyo tutaweka wazi kila kitu mara baada ya kukamilika usajili.”

Previous articleGUARDIOLA AWAPA ONYO MASTAA WAKE
Next articleSIMBA NA YANGA ZAKUTANA KWA NYOTA HUYU