GUARDIOLA AWAPA ONYO MASTAA WAKE

PEP Guardiola, Kocha Mkuu wa Manchester City amewapa onyo mastaa wake Jack Grealish na Phil Foden kutokana na tabia zao za kupenda bata wakati wanajua kwamba wanamajukumu kwenye timu.

Nyota hao wawili walishinda klabu usiku wakati wakijua kwamba kuna mchezo dhidi ya Newcastle United hali iliyopelekea kutoweza kupangwa kwenye mchezo huo.

Wakati City ikishinda mabao 4-0 dhidi ya Newcastle wikiendi nyota hao wawili walikuwa kwenye kikosi cha akiba na hakuna ambaye aliweza kuingia kucheza kati yao.

Ripoti zinaeleza kuwa nyota hao wawili walienda klabu usiku na walikuwa katika hali mbaya jambo ambalo lilimfanya Guardiola kuwaweka kando kwa kuwa alikasirika.

“Siyo kwamba niliamua kuwapumzisha tu wachezaji nilikuwa na maana yangu wanaocheza jua wanastahili na sio wengine.

“Kipindi cha krismasi ninakuwa makini na tabia za wachezaji ndani na nje ya uwanja kama wakiwa vibaya huko nje ina maana ndani wataharibu na wachezaji wanapaswa kuelewa kwamba anayekaa nje sio kwa bahati mbaya ila na tabia zinachangia,”.