YANGA YAWATUNGUA WAJELAJELA 2-1

TANZANIA Prisons leo Desemba 19 imekwama kuivunja rekodi ya Yanga kucheza mechi tisa bila kufungwa baada ya kupoteza mchezo wa Ligi  Kuu Bara.

Baada ya dakika 90, ubao wa Uwanja wa Nelson Mandela umesoma Tanzania Prisons 1-2 Yanga.

Bao la Samson Mbangula lilikuwa mapema kabisa dakika ya 9 kwa kichwa na liliweza kusawazishwa na Feisal Salum dk ya 23.

Khalid Aucho aliweza kupachika bao la ushindi dakika ya 43 alipokuwa akipambana na beki wa Prisons aliyekuwa akipambana kuokoa mpira wa Said Ntibanzokiza

Mabao yote matatu yalipatikana kipindi cha kwanza kwa kuwa ndani ya dakika 45 yalifungwa na kipindi cha pili mambo yalikuwa magumu kwa timu zote mbili.

Jeremia Juma hakuwa na bahati mbele ya Diarra Djigui kwa kuwa majaribio yake yote yalikwama mbele za mabeki pamoja na kipa Diarra.

Yanga inafikisha jumla ya pointi 23 kwenye msimamo ikiwa ipo nafasi ya kwanza na haijfungwa mpaka wakati huu.