DAKIKA 45, PRISONS 1-2 YANGA

DAKIKA 45 za mwanzo Uwanja wa Nelson Mandela timu zote mbili zimekwenda mapumziko huku Yanga wakiwa mbele.

Ni bao la Samson Mbangula wa Tanzania Prisons lilikuwa la kwanza kuwekwa kati dakika ya 9 kisha Salum Feisal alisawazisha dakika ya 23.

Dakika ya 43, kiungo Khalid Aucho alifunga bao la pili la kuipa uongozi timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Kwa sasa Prisons wanakwenda kujiuliza namna gani wanaweza kupindua meza na kupata ushindi huku Yanga wao wakienda kujiuliza namna gani watalinda ushindi wao.

Ubao unasoma Prisons 1-2 Yanga ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.