Home Sports KOCHA GEITA GOLD ATEMBEZA BONGE LA MKWARA

KOCHA GEITA GOLD ATEMBEZA BONGE LA MKWARA

BAADA ya kupata ushindi wa kwanza kwenye ligi kuu kocha wa Geita Gold FC Fred Felix Minziro amefunguka kuwa kwa sasa timu hiyo itaendeleza kupata ushindi kwenye michezo inayokuja mbeleni.

Minziro alisema aliichukua timu ikiwa kwenye wakati mgumu ikipata michezo migumu wakiwa ugenini ambayo yote walipoteza wakiwa viwanja vya Dar na waliporudi nyumbani wakapata alama tatu.

Akizungumza na Championi Jumatatu Minziro alisema kupata pointi hizo tatu kwake kuna maana kubwa sana kwa sababu kumewaongezea kujiamini na kuona kuwa inawezekana kwao kupata alama kwenye kila mchezo.

“Timu yangu sasa itaingia kwenye fomu ya kupata ushindi, kama ambavyo unajua nilichukua timu na tukapata michezo migumu tukiwa Dar es salaam. Tulivyorudi nyumbani pointi tatu zimepatikana.

“Kuna wachezaji wapya wameingia kwenye timu, hilo nalo litaongeza kitu kwenye kikosi na naona sasa tunaenda kufanya vizuri kwenye michezo yote, tukianzia hapa kwetu, lazima tuondoke na alama tatu kwanza hapa,” alisema Minziro.

Geita wamecheza mechi nane, wakiwa na pointi tano, ushindi mechi moja, sare mbili na kufungwa michezo mitano

Previous articleSUALA LA UWANJA, YANGA WAIJIBU SIMBA
Next articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO