>

BEKI WA KAZI KUSAJILIWA YANGA KUONGEZA NGUVU KWA JOB

UONGOZI wa Yanga umefunguka kuwa kuna uwezekano mkubwa wakaingia sokoni na kusajili beki mmoja wa kati mwenye uwezo mkubwa ili kuwa msaada kwa Dickson Job na Bakari Mwamnyeto ambao ndiyo tegemeo kwa sasa.


Hayo yalisemwa na 
Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Thabiti Kandoro alipokuwa anaweka wazi
mipango ya timu hiyo kwenye 
dirisha dogo la usajili ambalo limefunguliwa Desemba 16,
mwaka huu na kutarajiwa 
kufungwa Januari 15, mwakani.


Akizungumza na
 Spoti Xtra, Kandoro alisema viongozi wametazama kikosi na kupitia ripoti ya mwalimu,
wamegundua ili kudumu 
kwenye ubora walionao sasa ni vema wakasajili beki mmoja wa kati.


“Tunahitaji kuwa na timu 
iliyotimia kwenye kila idara, ukitazama kwa umakini utagundua Yanga inahitaji
kuwa na beki mwingine wa 
kati, kariba ya kina Mwamnyeto na Job.


“Lengo likiwa ni 
kuwapunguzia mzigo mzito wale wachezaji, hiyo itasaidia timu kuwa na ubora ule ule ambao sisi tunahitaji kuona kwenye kila mechi,” alisema.