SALAH HANA JAMBO DOGO ULAYA

MOHAMED Salah raia wa Misri, mshambuliaji wa Liverpool hana jambo dogo akiwa uwanjani kwa kuwa amekuwa ni mtu wa kazikazi.

Rekodi zinaonyesha kuwa amecheza jumla ya mechi 162 na ni mechi 155 alianza kwenye kikosi cha kwanza.

Katika mechi hizo jumla ya mechi saba alifanyiwa mabadiliko kutokana na sababu mbalimbali.

Akiwa ametupia mabao 110 ni mabao 15 katika hayo amefunga kwa penalti na kwa sasa ni namba moja kwa utupiaji ndani ya Ligi Kuu England akiwa ametupia mabao 15.