Home Sports NTIBANZOKIZA AIPIGA MKWARA SIMBA

NTIBANZOKIZA AIPIGA MKWARA SIMBA

SAID Ntinbanzokiza, kiungo mshambuliaji wa Yanga ameweka wazi kwamba watapambana kwa jasho bila kuchoka ili kuweza kupata ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Ni Simba ambao ni mabingwa watetezi huku Yanga wakiwa kwenye kasi ya kuufukuzia ubingwa hni nafasi ya kwanza kwenye msimamo na pointi zao ni 23 baada ya kucheza mechi 9 msimu wa 2021/22.

Ntibanzokiza amesema kuwa wanatambua kwamba mashabiki wanahitaji kuona timu inashinda jambo ambalo wanalifanyia kazi kila wawapo kwenye majukumu yao.

“Bado mapambano yanaendelea na tutapambana kwa jasho kupata ushindi ili kufikia lengo la kutwaa ubingwa, haitakuwa rahisi lakini mipango inaendelea kufanyika.

“Mashabiki wanapenda kuona sisi tunashinda mechi zetu hil hata sisi tunalipenda  pia kwani ili kupata pointi tatu ni lazima kushinda pale ambapo tunacheza tunaamini kwamba tutafanya vizuri,”.

Katika mabao 14 ambayo yamefungwa na Yanga kiungo huyo ametupia mabao mawili na ana pasi moja ya bao.

Previous articleSIMBA:TUTAFANYA USAJILI WA MAANA
Next articleUSAJILI UNAHITAJI UMAKINI,WAAMUZI MNA KAZI A KUFANYA