Home Sports SIMBA:TUTAFANYA USAJILI WA MAANA

SIMBA:TUTAFANYA USAJILI WA MAANA

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa kwenye dirisha dogo la usajili watafanya usajili wa maana kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco.

Dirisha dogo la usajili limefunguliwa Desemba 16 na linatarajiwa kufungwa Januari 15,2022 ambapo kwa sasa timu zimeanza harakati za usajili.

Akizungumza na Championi Jumatatu,Mwenyekiti wa Simba, Murtanza Mangungu alisema kuwa mipango ipo na wanahitaji kufanya jambo zuri kwa ajili ya timu hiyo.

“Tunajua kwamba wengi wanataka kusikia tutafanya nini kwenye wakati huu wa usajili, hatuna presha na jambo lolote,tutafanya usajili wa maana na mzuri.

“Kikubwa ni kuwa na subira unajua mambo mazuri hayahitaji haraka na kwa na kila kitu kinahitaji mikakati imara,” alisema Mangungu.

Previous articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE
Next articleNTIBANZOKIZA AIPIGA MKWARA SIMBA